Wizkid awatelekeza mashabiki wake kwenye mvua, Zimbabwe

MWANAMUZIKI maarufu wa Nigeria, Wizkid, hivi majuzi aliwaudhi mashabiki wa Zimbabwe baada ya kutotumbuiza nchini humo katika ziara yake ya kwanza kutokana na mvua ambayo ilinyesha na kukatisha uhondo huo.
Mashabiki walimsubiri nyota huyo kutoka saa moja jioni usiku hadi saa nane katika kiwanja cha michezo ambako kutokana na kutofanyika kwa tukio hilo mashabiki walifanya fujo na kuharibu vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurusha chupa tupu za vinywaji.
Katika akaunti mbalimbali za mashabiki hao, waliandika kumshutumu mwanamuziki huyo kijana wakimuuliza alijisikiaje kulipwa ‘minoti’ bila ya kufanya shoo yoyote

No comments

Powered by Blogger.