Kisa Kuvaa Hereni, Diamond Ashambuliwa Mtandaoni

MFALME wa Bongo Fleva nchini anayekimbiza na ngoma yake ya Make Me Sing, Diamond Platnumz amejikuta kwenye wakati mgumu huku akishambuliwa kwa maneno kwenye mtandao wa Instagram baada ya jana Jumatano kuweka picha iliyomwonesha akiwa amevaa hereni.
Picha hiyo ilizua sintofahamu kwa mashabiki zake huku wengi wao wakihoji imekuwaje na nini kimemsibu staa huyo kutoboa pua na kuvaa hereni. Ikumbukwe kuna wimbo wa Muziki Gani ambao Nay wa Mitego alimshirikisha Diamond na ndani yake kuna maneno ambayo Diamond ameimba ‘kuwaponda’ wasanii wa hip hop kwamba kazi yao ni kutoboa pua. Kipande cha msitari “kazi yenu kutoboa pua”. Hii ilisababisha baadhi ya mashabiki walitaka afafanue hilo.
Wengine waliandika wakionesha kushangazwa na kitendo cha kutoboa pua na kuvaa hereni ilihali Diamond ni muumini wa dini ya Kiislam, kwa maadili ya Kiislam mwanamme haruhusiwi kutoboa pua, wala masikio wala kuvaa hereni. Kwa mujibu wa komenti za mashabiki, Diamond ameoonekana kukiuka maadili ya dini yake kwa kuvaa hereni na kuchora tatuu.
source global publishers

No comments

Powered by Blogger.