Taylor Swift amshauri Selena Gomez kupata ‘boifrendi’ wa ukweli
Staa wa Pop, Taylor Swift akiwa na shosti yake Selena Gomez.
LOS ANGELES, Marekani
STAA wa Pop, Taylor Swift yupo kwenye furaha juu ya uhusiano wake, lakini anataka kuona rafiki yake wa ukweli, Selena Gomez naye akiwa kama yeye hivyo amempa ushauri wa namna ya kumpata mpenzi atakayempa furaha kama ilivyo kwake na Calvin Harris.
Chanzo kimesema, Selena, 23, amekuwa akijiona kama hana bahati tangu alipoachana na Justin Beiber lakini ‘bestie’ Taylor, 25, anataka kuhakikisha anakuwa na furaha kwa kumshauri kuwa anatakiwa kuwa na amani na muda utakapofika basi atapata mwenza wake ambaye atakuwa anaendana naye na watakuwa na furaha.
“Taylor amekuwa akimpa moyo sana Selena. Amemtaka awe na amani. Cha muhimu zaidi amemtaka aufungue moyo wake na akili na alimwambia siri ya kutafuta mwanaume mzuri kama ilivyo kwake alivyomnasa Calvin,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Selena anataka kufanya kila kitu ili kuhakikisha anapata mwanaume ambaye atahakikisha uhusiano wake unakuwa kama wa rafiki yake Taylor na Calvin.”
Selena ambaye pia ni msanii wa muziki pia alikuwa mmoja kati ya nyota waliomtakia heri Taylor kwenye sikukuu yake ya kutimiza mwaka mmoja akiwa kwenye uhusiano na Calvin.

No comments