Dayna na Kasimulizi ka’ rushwa ya Ngono

Stori: Andrew Carlos
Mdada anayefanya poa na ngoma yake ya Angejua, Dayna Nyange ametoa kasimulizi f’lani amaizing kuhusu jinsi wasanii wa kike wanapojikuta kwenye mtego wa kutakiwa kutoa rushwa ya ngono ili wapate mameneja.
IMG_1965Dyana alisema: “Unajua mimi ni mtoto wa kike, unaweza kukuta jamaa kanipenda lakini kwa ugumu wangu anatumia mbinu ya kutaka kunimeneji kimuziki.
“Sasa na mimi nahitaji sapoti hiyo? Nikikubali ataanza kiniweka karibu, atanihudumia halafu baadaye nikishapendeza sana ataniletea mambo hayo, kama huna msimamo unaweza kuingia kwenye mtego lakini mimi mambo hayo kwangu mwiko,” alisema Dayna.

No comments

Powered by Blogger.