Hakuna Haja ya Korabo na Wanaijeria – JB
MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’
amesema kuwa haoni sababu ya kuigiza filamu kwa kuwashirikisha wasanii
wakubwa kutoka Naijeria au Ghana ili kupata sinema kubwa bali ni kutumia
kampuni kubwa za filamu kutoka afrika ya Kusini kufanya nao kazi.
“Hakuna haja ya kuwashirikisha wasanii kutoka Naijeria au Ghana ili kufanya filamu kubwa, Marehemu Kanumba alifanya hivyo kwa wakati ule ilikuwa ni wakati wake, sasa watu wanataka sinema kubwa kutoka kwetu,”JB
Aidha amesema kuwa anathamini mchango wa marehemu Kanumba kuitangaza filamu nje lakini toka kuondoka kwake hakuna aliyefanikiwa kufanya vizuri kuwashirikisha wasanii kutoka nje kwani alikuja Van Vicker kucheza filamu ya Never give up na Hashim Kambi na haikuwa filamu kubwa, JB anaamini kuwa filamu kubwa itatengenzwa na Jerusalem company.

No comments