Zari ‘Mama Tiffah’: Nafuata Dini ya Mpenzi Wangu


BAADA ya sintofahamu nyingi kuibuka katika mitandao ya kijamii kuhusiana na picha za mpenzi wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zari the boss Lady, kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akibatizwa mtoni, mwenyewe ameibuka na kuweka sawa sintofahamu hizo.
Akizungumza na mtangazaji, Millard Ayo kupitia kipindi cha Top Twenty, Zari alikubali kuwa picha hizo ni kweli zinaonyesha tukio la kweli la kubatizwa kwake lakini ilikuwa mwaka 2013 huku akishangazwa na usambazaji wa picha hizo kwa mwaka huu wa 2016.
“Nikweli nilibatizwa na kuwa Mkristu ilikuwa mwaka 2013, lakini sasa nina maisha mengine nimefuata dini ya mpenzi wangu, Diamond, nashangaa kwa nini picha hizo za mwaka huo ziwe stori leo wakati ni muda mrefu na sasa nina maisha yangu mengine,” alisisitiza Zari.
Aliongeza kwamba, licha ya kuwa na maisha yake mapya anaendelea na mambo yake mengine kwa kuwa yupo na maisha mapya hivyo anafuata dini ya mpenzi wake huyo ambaye ni maarufu na nyota katika muziki wa Bongo Fleva nchini huku akiwa na idadi kubwa ya tuzo zinazotokana na umahiri wa muziki wake.

Mtanzania

No comments

Powered by Blogger.