Batuli Kuja Kivingine Baada Ya Uchaguzi

Muigizaji wa filamu, Batuli amesema amejipanga kuja tofauti katika filamu zake baada ya kujifunza mambo mengi kutoka kwenye kampeni za uchaguzi alizoshiriki.

Batuli ameiambia Bongo5 kuwa atafanya kazi kubwa ili kuhakikisha kazi zake zinagusa maisha ya watanzania wa kawaida aliowaona wakati akizunguka kwenye kampeni za CCM.

“Nakuja kivingine kwa sababu nimejifunza mengi kwenye kampeni na kuna umuhimu wa kuviweka kwenye kazi zangu,” amesema. “Nitafanya filamu za kibongo kama kawaida lakini zenye maudhui tofauti na pia zina ujumbe tofauti na maisha ya kawaida kutokana na ambacho nimekisoma.”

“Unajua kile kipindi cha nyuma sikuwa mwanasiasa lakini sasa hivi ni mwanasiasa, lakini sisi wote tunatetea jamii kwa njia moja au nyingine, tunatakiwa kufanya hivyo kutumia kazi zetu,” ameongeza.

Bongo 5

No comments

Powered by Blogger.