Young Thug anasemaje kuhusu kupenda kuvaa nguo za kike? Mapenzi ya jinsia moja je!?
Msanii wa muziki wa rap kutoka Marekani, Young Thug
 anajulikana kwa kazi zake nyingi za muziki lakini pia anajulikana zaidi
 kwa tabia yake ya kupenda kuvaa nguo za kike, kitu ambacho kimeleta 
maneno mengi sana juu ya rapper huyo huku wengi wakidai pengine labda 
rapper huyo anachochea mahusiano ya jinsia moja!
Kwa muda mrefu sana Young Thug
 amekuwa akisita kufanya interviews na Radios pamoja na majarida 
mbalimbali kuhusu vitu hivi, lakini hivi karibuni rapper huyo alikubali 
kufanyiwa interview na jarida la The Guardian,
 na miongoni ya maswali alioulizwa ni kwa nini anapenda sana kuvaa nguo 
za kike na je anavutiwa na wanawake ama wanaume zaidi! Rapper huyo 
alikuwa na haya ya kusema…
>>>
 ” Kwanza napenda kuvaa nguo za kike kwa sababu zinanikaa freshy sana, 
nguo za kike zinakuja kwenye size ileile nayoitaka mimi haswa jeans, 
jeans zangu zote ni za kike hata hii nilioivaa na kama kuna kitu 
chochote cha kiume kwenye kabati langu la nguo basi itakuwa ni T-shirt 
zangu na raba tu lakini asilimia 99 ya nguo kabatini mwangu ni  nguo za 
kike… “<<< Young Thug.
Alipoulizwa anavutiwa na jinsia gani zaidi kimapenzi, rapper huyo alikuwa na haya ya kusema…
>>>
 “navutiwa kusikiliza kila kitu ambacho watu wanasema na kukiongelea juu
 yangu, haijalishi wanasema nini. Niwe napenda watu wa jinsia moja, niwe
 kichaa, niwe na demu mkali, niwe mbaya, labda waseme sijui kurap… vyote
 mimi naenjoy kuvisikiliza tu, nawaacha waongee.” <<< Young Thug.
Design kama Young Thug
 alikwepa kujibu swali hilo kwa kudai kuwa yeye anasikiliza tu maneno 
yote yanayozungumzwa na watu juu yake, lakini kitu ambacho amekiweka 
wazi bila kuficha ni kwamba, yes anapenda kuvaa sana nguo za kike kwa 
sababu zinamkaa vizuri mwilini!


No comments