Rose Ndauka Aamua Kuwekeza Huku

Msanii maarufu wa filamu, Rose Ndauka ameamua kujitosa kwenye muziki kwa kuanzisha kundi la vijana wenye vipaji litakalosimamiwa na kampuni yake ya Rosie.
Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Rose amesema licha ya vijana hao kutunga wimbo wa kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi, kundi hilo linaendelea kufanya kazi za muziki.
“Hiki ni kipindi cha uchaguzi, kwahiyo nikasema nitashiriki vipi mimi kama msanii kuwaelimisha Watanzania wenzangu ili tuwe na amani yani tuwe sawa? Kwa sababu inaoneka hiki kipindi kumekuwa na machafuko, kwahiyo nikataka na mimi kushiriki kwa namna moja au nyingine. Nikasema njia pekee ambayo mimi naweza kushiriki nikawaambia vijana wangu tungeni nyimbo ambayo inahamasisha amani Tanzania kwa kipindi hiki cha uchaguzi tukaingia studio,” alisema Rose.
Licha ya kufanya muziki, Rose alisema kundi hili pia lina vijana wenye vipaji vya kuigiza na vingine.

Chanzo: Bongo 5

No comments

Powered by Blogger.