mbinu zinazomfanya GUADIOLA aendelee kung'ara ujerumani


 Bayern Munich walisherehekea siku ya mwisho ya ‘OktoberFest’ siku ya jumapili kwa kuiadhibu Borussia Dortmund 5-1, ushindi wao mkubwa zaidi dhidi ya Ruhr tangu kabla ya ushindi wa BVB wa Bundesliga mara mbili mfululizo katika misimu ya 2011 na 2012.
Wengi wameuelezea ushindi huo kama ndio mwisho wa msimu wa 2015/16, huku Bayern wakitawazwa kuwa mabingwa ndani ya miezi miwili tu, na kuna sababu ya kuamini hilo. 
 Kipigo cha wikiendi hii kinawaacha Dortmund pointi 7 nyuma ya Bayern. Schalke, ambao nao walifungwa 3-0 na Koln mapema wikiendi iliyopita, wapo nyuma kwa pointi 8. Washindi wa pili wa ligi msimu uliopita nao wapo nyuma kwa pointi 12 katika nafasi ya tisa baada nao kuadhibiwa na Bayern 5-1 kama ilivyokuwa kwa BVB siku ya jumapili.
Bayern wameshinda mechi zote katika mashindano yote tangu walipopoteza mechi ya DFL Superpokal, mechi yao ya kwanza ya ushindani msimu huu, lakini mpaka kufikia sasa inaonekana wazi hakuna timu barani ulaya sio tu Ujerumani inayoweza kuzidi kiwango chao cha hivi sasa.
Kuna sababu kadhaa za kuimarika kwa kiwango cha Bayern katika kuelekea kuitawala tena soka la ulaya.
  Mojawapo ya sababu hizo ni kiwango cha Robert Lewandowski, ambaye amefunga magoli 12 katika mechi 4 zilizopita. Sababu nyingine ni ubora wa kiungo mpya Douglas Costa, ambaye ametoa pasi ya goli au magoli katika kila mechi ya Bundesliga kabla ya mchezo dhidi ya BVB.
  Na inasaidia sana ukiwa na aina ya wachezaji wa daraja la dunia, pia Thomas Muller na Jerome Boateng, wote wakiwa wana umri kati ya 25 mpaka 27, wakiwa na uzoefu mzuri na katika kiwango cha juu cha maisha yao ya soka.
  Ukiachana na ubora wa mchezaji mmoja mmoja, Pep Guardiola anastahili sifa kwa mabadiliko ya kifundi. Hatimaye sasa anaonekana amepata mzuri ambao unamuwezesha sio tu kushinda mechi mechi bali pia kupata ubora wa wachezaji wake mmoja mmoja.
Katika misimu yake miwili ya kwanza ndani ya Allianz Arena, mafanikio ya Guardiola katika Bundesiliga yaliyoa uhakiki wa uongo juu ya mbinu zake.
Kushinda ubingwa kwa rekodi ya aina yake msimu wa 2014 ulitoa ishara kwamba timu yake ilikuwa ikicheza katika ubora wake, lakini timu hiyo hiyo iliposhiriki katika Champions League haikuwa kwenye ubora waliokuwa nao nyumbani.
Na pamoja na kwa mara nyingine tena kubeba ubingwa kirahisi nyumbani mwaka 2015, Bayern bado walikuwa na matatizo makubwa katika ‘Big Matches’. Walipata taabu kabla ya kutolewa katika DFB-Pokal na Champions League, na hata kwenye Bundesliga walikuwa na rekodi mbaya dhidi ya timu sita za juu.
  Bayern msimu huu wamekuwa tofauti kabisa na Bayern ya misimu miwili iliyopita. Wamekuwa wakidhiadhibu vizuri mno timu kubwa kama Dortmund, Wolfsburg na hata Bayern Leverkusen, wakati wakipata taabu kidogo katika mechi zao za ushindi dhidi ya Hoffenheim na Augsburg. Yote haya yamesababishwa na kiasi kikubwa na mabadiliko yenye kujali mahitaji ya timu kulingana na wachezaji ilionao.
Dhidi ya Dortmund, Philipp Lahm na David Alaba walirudi kucheza kwenye nafasi zao halisi kwenye nafasi za ulinzi wa pembeni. Wote wameiimarisha sana timu msimu huu wakiwa kwenye nafasi walizozioea, Guardiola alikuwa akiwatumia kwenye safu ya kiungo mwanzoni. Bayern waliingia dimbani vs BVB wakiwa na mabeki wanne nyuma ambao walikuwa na sapoti kutoka kwa mawinga.
Huko nyuma, Guardiola mara nyingi alikuwa akipenda kucheza na mshambuliaji wa kati asiye halisi ‘false 9′, Muller au Gotze wakicheza mbele. Ubora wa Lewandoski wa hivi umemfanya Guardiola akose namna zaidi ya kumchezesha mshambuliaji halisi katika nafasi yake.
  Kuliko kucheza kwa kuubana uwanja, Pep hivi sasa anapendelea kucheza kwa staili ya kutanua uwanja, hasa baada ya kurudisha mfumo wa kucheza na mabeki na mawinga wanaosapotiana.
Huko nyuma, Bayern walikuwa wanafeli katika hatua fulani kutokana na makosa ya kiufundi ya Guardiola: Kuwatumia wachezaji nje ya nafasi zao halisi, kucheza kwa kuweka mtego wa offside au kuweka focus kubwa katika kumiliki mpira na kukosa kasi ya mcheo na pia matumizi ya kutanua uwanja katika mashambulizi.
Dhidi ya timu dhaifu, Guardiola na mbinu zake hizi alifaulu: Kasi na nguvu za Boateng ziliwazidi washambuliaji wengi lakini kucheza kwa kwa mtindo wa man-marking dhidi ya washambuliaji hatari zaidi duniani huku ukiwa na ukuta wa mabeki watatu wanaocheza karibia na mstari wa safu ya kiungo usingeweza kufanikiwa hata kidogo, na kwa hakika zaidi mbinu hizi za ufundi hazikupaswa kutumika na Guardiola dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya Champions League msimu uliopita.
Guardiola alirithi kikosi kilichoshinda makombe matatu na labda alikuwa na presha ya kuendeleza mazuri ya aliyemrithi. Ilifikia pointi alikuwa anajaribu kutambulisha mbinu mpya ili mradi tu ni mbinu mpya, alikuwa anajaribu kuunda Bayern itakayocheza kwa namna tofauti kabisa na mtangulizi wake.
Mambo yamebadilika sasa na Guardiola amebadilika zaidi kimbinu na kujali zaidi matokeo ya mwisho.
Wachezaji wake wakiwa mchanganyiko ya waliokuwepo katika ushindi wa makombe matatu mwaka 2013 na wapya wenye sifa zinazofanana, na staili ya mchezo inafanana mno na ile aliyokuwa anatumia Jupp Heynckes.
Hitaji la kumiliki mpira limeshuka, hivi sasa Bayern wanamiliki mpira kwa wastani wa 55.7% kwa mechi, hivi sasa msisitizo wa mchezo aao upo katika kasi katika kutoka kwenye ulinzi mpaka kwenye mashambulizi.
Staili hii ya mchezo ilisababisha magoli mawili dhidi ya Dortmund – Boateng aki-supply pasi kwa Muller na Lewandoski, goli la kwanza na la tatu. Hii ni timu ya Guardiola na mbinu zake lakini zenye kukidhi hitaji la ushindi zaidi kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.
Guardiola kuachana na misingi yake, ameamua kubadilika na kukubali kutumia mbinu zenye kuendana na mahitaji.
Bayern walionyesha wazi nini wanamaanisha juzi jumapili na inaonekana wazi kwa sasa hakuna timu yenye kiwango kinachokaribia cha Bayern. Ikiwa wataendelea kucheza kwa kiwango hiki mpaka kufikia Mwezi May 2016, basi naiona historia mpya ikitengenezwa ya kubeba vikombe vyote wanavyoshindania.

No comments

Powered by Blogger.