Kabla ya kupata mafanikio katika soka, hizi ni kazi za kwanza kufanya mastaa hawa Di Maria, Zlatan, Ribery na Sanchez
Katika maisha kuna mambo mengi ya
kupitia hadi kufikia mafanikio mara nyingi au kwa asilimia kubwa wengi
waliofanikiwa katika maisha walihangaika kufikia kilele hicho cha
mafanikio kiasi hata cha kufikia kuwa mfano mzuri kwa vijana
wanaohangaika kusaka mafanikio katika soka. October 11 naomba
nikusogezee kazi za kwanza za mastaa hawa wa soka.
1- Angel Di Maria ni mchezaji ambaye wengi tumeanza kumfahamu vizuri kupitia vilabu vya Real Madrid na Manchester United kabla ya dirisha la usajili la mwezi August alipoamua kujiunga na PSG ya Ufaransa, unaweza ukafikiria ametokea katika familia ya kitajiri ila Di Maria amewahi kufanya kazi katika sehemu ya kuhifadhia makaa ya mawe akiwa yeye, wazazi wake pamoja na dada zake Vanesa na Evelyn lakini leo hii ni staa na tajiri mkubwa kupitia soka.
2- Zlatan Ibrahimovic
akiwa na umri wa miaka 15 alikaribia kuachana na soka na kutaka
kutafuta maisha kwa njia nyingine kabla ya meneja wake kumshawishi
asifanye maamuzi hayo, Zlatan
alikuwa akiacha kucheza soka na kwenda kufanya kazi katika vivuko vya
pwani ili apate fedha ya kujikimu. Lakini sasa anatajwa kuwa moja kati
ya wachezaji bora duniani.
3- Alex Sanchez mshambuliaji wa kimataifa wa Chile anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza ambaye amewahi kutamba katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania. Sanchez kabla ya kuanza kupata mafanikio katika soka aliwahi kufanya kazi ya kuosha magari kabla ya soka kuwa mkombozi wa maisha yake.
4- Carlos Bacca ni mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia na klabu ya AC Milan ya Italia
ambaye kabla ya kuanza kupata mafanikio alikuwa mvuvi kwa kipindi
kirefu kidogo na alikuwa msaidizi wa dereva, mpira ulikuwa kama sehemu
ya kujifurahisha, historia yake inaonyesha katokea mtaani na kuanza
kucheza soka katika timu ya Atlético Junior.
5- Frank Ribery ni winga wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, amewahi kupitia misukosuko mingi katika maisha yake, akiwa na umri wa miaka miwili Ribery alipata ajali ya gari pamoja na familia yake kitu ambacho kimemfanya abaki na makovu usoni hadi leo hii, Ribery aliwahi kufanya shughuli za ujenzi pamoja na baba yake, yote hiyo ilikuwa ni katika harakati za kutafuta maisha.
No comments