Kabla ya kujaribu bahati yake kwa Lil Wayne, Drake aliomba asimamiwe na staa huyu…
Mkurugenzi wa Konvict Muzik na lebo ya KonLive, Akon anajulikana kwa kuwatoa kimuziki wasanii wakubwa Marekani baadhi wakiwa T-Pain na Lady Gaga ambao uwezo wao dunia nzima inashuhudia… lakini ulikuwa unajua kuwa Akon alikataa kumsimamia Drake kipindi hicho rapper huyo anahangaika kutoka kimuziki!? sababu zake?
Akiwa kwenye interview na Montreality online TV ya Marekani, Akon aliulizwa kwa nini aligoma kumsimamia Drake kipindi hicho na je anajutia maamuzi hayo sasahivi? Akon alikuwa na haya yakusema…
>>> “Kweli
kipindi hicho nilikataa kumsimamia Drake kwasababu alikuwa tofauti sana
na jinsi alivyo sasahivi… kwa mfano wimbo wa ‘The Best I Ever Had’
ulikuwa tofauti sana kipindi kile anaileta demo hiyo kwangu. Nadhani
alikuwa bado anatafuta sauti yake na aina ya muziki ambao angependa
kuufanya… lakini kwa wakati ule Drake hakuonekana kama biashara nzuri
kwangu wala lebo yangu… alikuwa muoga sana na mwenye aibu kubwa, siwezi
kusema najutia maamuzi yangu ila kwa kipindi kile sikuona kama
angeniletea faida kifedha ila kadri miaka ilivyokwenda confidence ya
Drake ilikua sana, hata akiwa on stage unaweza kuona kuwa amekua sana
kimuziki, amejifunza kuimiliki audience kwa asilimia mia, he is good”. <<< Akon.
Licha ya Drake kukataliwa na Akon msanii huyo aliendelea na safari yake ya muziki na sasa hivi ni miongoni wa masataa wenye majina makubwa kwenye muziki wa HipHop Marekani akiwa chini ya Cash Money Records ya kwake Birdman na Lil Wayne.
No comments