HAWA NDIO WACHEZAJI WATANO WATUKUTU KWENYE HISTORIA YA EPL
Mshambuliaji wa Chelsea Diego 
Costa ametajwa kuwa mchezaji mwenye tabia chafu zaidi katika ligi kuu 
Uingereza msimu huu, baada ya kuondoka kwa Mario Baloteli na Joey 
Barton.
Lakini mbali na Costa hii ndio 
listi ya wachezaji wengine waliowahi kuwa na tabia kama hizo kuwahi 
kutokea katika historia ya EPL katika nyakati tofauti tofauti.
5. Scott Parker
Kiungo huyu wa Kiingereza 
amejikusanyia kadi takribani 86 za manjano katika muda wote aliocheza 
ligi kuu Uingereza akiwa na vilabu vya Chelsea, Newcastle United, West 
Ham United,Tottenham Hotspur na Fulham(kabla haijashuka daraja).
4. Patrick Vieira
Alisajiliwa na Arsenal akitokea
 kunako klabu ya Inter Milan, kiungo na nahodha huyo wa zamani wa 
Arsenal, alikuwa ni mpinzani mkubwa wa nahodha wa zamani wa Manchester 
United Roy Keane ambaye pia alisifika kwa tabia chafu.
Licha ya kubeba makombe matatu 
ya EPL likiwemo lile ambalo walimaliza ligi bila ya kufungwa , Vieira 
ndiye nahodha pekee wa Ligi Kuu Uingereza kupata kadi mbili za manjano 
katika matukio sita kwenye mchezo mmoja na kuonyeshwa kadi mbili 
nyekundu. Katika kipindi chote cha maisha yake ya soka Vieira alipenda 
sana migongano na wachezaji wenzake kama Roy Keane.
3. Kevin Davies
Huyu ni nahodha wa zamani wa 
Bolton Wanderers amefanya na kufanyiwa faulo nyingi zaidi katika 
historia ya Ligi Kuu nchini Uingereza.
Alicheza katika klabu kadhaa katika miaka yake 22 ya maisha yake ya soka zikiwemo Southampton, Bolton Blackburn Rovers.
2. Paul Scholes
Kiungo huyu wa zamani wa 
Manchester United ni mchezaji wa tatu kwa kuonyeshwa kadi za njano 
nyingi zaidi katika historia ya Ligi Kuu Uingereza nyuma ya mshambulizi 
wa zamani wa Bolton Kevin Davies na kiungo wa zamani wa Newcastle Lee 
Boywer.
1. Vinnie Jones
Huyu unaweza kumwita mchezaji 
mgumu kuliko kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka, Jones anashikilia 
rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kupewa kadi kwa haraka zaidi 
katika mchezo rasmi, akipewa kadi baada ya sekunde tatu tu kwenye mchezo
 wa kuwania kombe la FA mwaka 1992 wakati akikipiga kunako klabu ya 
Chelsea.
Jones ametolewa nje katika 
matukio sita tofauti katika Ligi Kuu nchini Uingereza, akizawadiwa jumla
 ya kadi nyekundu 12 katika maisha yake yote ya soka na kufunga ukurasa 
wa wachezaji wenye nidhamu mbovu zaidi katika mchezo wa soka kunako Ligi
 Kuu Uingereza 

No comments