Du!!! kabla ya kuanza kuifundisha Liverpool, Jurgen Klopp kaanza kuiingizia mkwanja Liverpool (+Picha)
Ikiwa ni siku moja imepita toka klabu ya Liverpool wamtambulishe kocha wao mpya Jurgen Klopp mbele
ya waandishi wa habari na kuanza kufanya mahojiano na kocha huyo wa
Kijerumani, mengi yaliandikwa ila kauli yake imegeuka fursa ya
kibiashara na tayari imeanza kuzalisha fedha.
Jurgen Klopp ambaye hadi anaondoka katika klabu ya Borussia Dortmund
alikuwa na heshima kubwa kutokana na mambo mazuri aliyoifanyia klabu
hiyo, licha ya kuwa nyakati za mwishoni hakuwa akifanya vizuri na timu
kiasi cha kushika nafasi za chini katika msimamo wa Ligi Kuu Ujerumani. Kama
ambavyo tumezoea kuona mchezaji mpya au kocha mpya akitambulishwa huwa
kuna interview fupi pamoja na kuongea na mashabiki wa klabu husika.
Kwa upande wa Jurgen Klopp alizungumza kauli kadhaa ila moja kati ya kauli alizoongea kuwa yeye ni kocha wa kawaida na angependa aitwe ‘the normal one’ ni jina ambalo tofauti kidogo na kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambaye hupenda kujiita ‘the special one’. Jina hilo ambalo angependwa kuitwa limeandikwa katika fulana na kuanza kuuzwa kwa mashabiki wa Liverpool, ikiwa ni chini ya masaa 24 toka atamke kauli hiyo.
No comments